
Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA), Regina Mbaji
Mbaji amebainisha kuwa kupitia wao kufanya kazi kwa bidhii kutaondoa dhana potofu, iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuwa mlemavu hawezi kuwa kiongozi.
Aidha Regina Mbaji, amesema muda wa kufanya kazi umefika na akaipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuweka maandishi ya nukta nundu, ambayo yameongeza ufanisi na usiri kwa walemavu wasioona kuweza kupiga kura.
Pia Mbaji amesema, zipo changamoto kadhaa ambazo CHAWATA imezibaini hasa kwa wanachama wake ambao walishiriki kampeni, ikiwemo kushindwa kuzunguka kutokana na hali ya uchumi na mazingira ya ulemavu, huku akipendekeza uwepo wa jimbo ambalo litawahusu watu wenye ulemavu tu.