Mkurugenzi TAKUKURU Dkt Edward Hoseah
Matokeo hayo yametolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mtafiti mwandamizi kutoka Repoa Bi. Rose Aiko, ambapo umeonesha kuwa TAKUKURU imeshika nafasi ya nne kwa kuomba rushwa, polisi wakiwa wa kwanza, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa wa pili huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mahakama.
Kwa mujibu wa Bi. Aiko, wengi kati ya waliohojiwa katika utafiti huo wamesema kiwango cha rushwa nchini kimekuwa kikiongezeka na kwamba kumekuwa na mwamko mdogo wa watu kutoa taarifa punde wanapoombwa rushwa na watendaji kutoka moja ya taasisi zinazotajwa kuongoza kwa rushwa.