
Simba waliouawa
Mkuu wa Hifadhi ya Kipengere mkoani Njombe, Donasiani Makoye, amesema Simba hao walitoweka Hifadhini Julai 21 mwaka huu na wao waliendelea kuwafuatilia Simba hao na leo wamefanikiwa kuwaua
Mhifadhi huyo amekiri kuwa Simba hao wamesababisha madhara makubwa kwa kushambulia na kuua ng'ombe 14 na nguruwe 5.
Aidha Mhifadhi huyo Amesema wao Kama Jeshi la Uhifadhi wanaendelea kuchukua hatua zaidi ili kuwadhibiti Simba hao ikiwa pamoja na kuwafungia mfumo wa mawasiliano ya utambuzi
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Makungu wamesema kwa muda mrefu wameshindwa kuendelea na majukumu yao kwa kuhofia Simba hao.
Wananchi wamesema wanawashukuru Askari hao wa Hifadhi ya Kipengere