Ijumaa , 10th Jun , 2016

Serikali ya Tanzania imesema kuwa ipo mbioni kuleta sheria ambayo itasaidia katika kutokomeza tatizo la ajira kwa watoto katika maeneo mengi nchini.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Manajementi ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki ametoa kauli hiyo akijibu swali Bungeni lililouzwa katika kurekebisha mapungufu ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambapo ameeleza kuwa kwa sasa serikali inaandaa mkakati wa kuchukua maoni kutoka kwa wananchi kabla ya kurejeshwa bungeni.

Aidha, akizungumzia suala la watoto waliopo katika ajira za utotoni, Mhe. Angella amesema kumekuwepo na mkakati wa utoaji wa elimu kwa wazazi pamoja na kuwawezesha zaidi ya watoto 102,000 Zanzibar kwenda shule kupitia Mfuko wa TASAF.