Jumatano , 23rd Nov , 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi Ajira na Vijana) Bibi Jenista Mhagama amesema serikali itakaa na wadau ili kuangalia namna ya kulimaliza sakata la fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kutokea kushoto, Nicholaus Mgaya, katibu Mkuu TUCTA, Waziri Jenista Mhagama, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa MKoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo katika mkutano wa sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) mjini Dodoma uliofunguliwa leo na Waziri Mkuu Mjini Dodoma, ambapo katika risala yake, TUCTA ilihoji kuhusu  marekebisho ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na ucheleweshwaji wa malipo ya pensheni.

Mhagama amesema kuwa baada ya uongozi wa TUCTA kukamilika, itabidi wakutane na kukaa pamoja kuainisha sera inataka nini na hali ya uchumi ya sasa ikoje huku wakiangalia dhana nzima ya hifadhi ya jamii nayo inataka nini.

Jenista Mhagama

“Kuna haja ya kuangalia sera inataka nini, tunapaswa tuangalie mabadiliko ya kiuchumi katika nchi yetu na kutazama dhana nzima ya hifadhi ya jamii kwenye maisha yetu ya uzeeni. Tukikaa pamoja, yaani, mwajiri, mfanyakazi na Serikali, tutapata njia ya kisheria ya kuweza kulifunga jambo hili ili lisiendelee kuwa kero kwa wafanyakazi wetu,” alisema.

Msikilize hapa waziri Mhagama akifunguka.

Sauti ya Waziri Jenista Mhagama