
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa nchini Tanzania Dkt Hussein Mwinyi.
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kutaja fursa hizo kuwa ni kupitia miradi ya uzalishaji mali na huduma za ulinzi zinazotolewa na jeshi la kujenga taifa JKT.
Dkt Mwinyi amesema ni kwa kupitia miradi kama hiyo, vijana wanaojiunga na jeshi la kujenga taifa watajikuta wakipata fursa za ajira na kutolea mfano kitengo cha huduma za ulinzi cha jeshi hilo ambacho hivi sasa kinatoa ajira kwa idadi kubwa ya vijana.