Ijumaa , 26th Feb , 2016

Serikali imesema itawanyang'anya na kuwafutia vibali vya kuuza sukari nchini, mawakala iwapo watabainika kuficha bidhaa hiyo kwa lengo la kusababisha uhaba.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema wanaotaka kujua hatua gani zinazochukuliwa na serikali ni kwamba watafanya ukaguzi katika maghala ili kubaini walioficha sukari na kuwachukulia hatua.

Waziri huyo amesema mahitaji ya sukari kwa sasa ni tani 590 huku uwezo wa viwanda kuzalisha sukari ukiwa ni tani 320 akimaanisha kuwa kuna uhaba wa tani 250 ambazo zitapatikana kwa viwanda kuongeza uzalishaji.

Waziri Mwijage amesema amemuagiza mkurugenzi wa leseni ambaye ngazi ya halmashauri na wizara kuwaandikia barua mawakala wote wa sukari nchini na kuwatahahadharisha juu ya hatua zozote za kutaka kuficha sukari na jinsi ambavyo serikali halitalianyamazia hilo.

Baadhi ya wafanyabishara walidai hali hiyo imetokana na bei ya mfuko wa kilo 50 katika maduka ya jumla kwa sasa kuuzwa kati ya elfu 92,000 hadi 95,000 wakati awali walikuwa wakinunua sh. 82,000