Alhamisi , 13th Mar , 2014

Chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno nchini Tanzania, kwa kushirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jamii kinakusudia kuandaa mfumo wa ukauguzi na uhakiki wa dawa za meno ili kuona kama zinakidhi mahitaji ya matumizi ya binadamu.

Rais wa chama cha afya ya kinywa na meno ambaye pia ni daktari bingwa wa meno kwa watoto wadogo Dkt. Rachel Mhaville, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia ushiriki wa chama hicho katika siku ya kimataifa ya afya ya meno ambayo hufanyika machi 20 kila mwaka.

Dkt. Mhaville amefafanua kuwa zoezi hilo litakalohusisha wadau wa meno wakiwemo watengenezaji na waagizaji wa dawa wa ndani na nje, linalenga kuhakikisha kuwa dawa zote zinazouzwa madukani, zinakidhi vigezo vya kitaalamu ili kuondoa uwezekano wa dawa zisizo na viwango kuingia sokoni na hivyo kuleta madhara kwa watumiaji.