Selemani Jafo - Naibu Waziri TAMISEMI
Idadi ya ajira hizo itajumuisha walimu waliohitimu masomo ya Ualimu kwa mwaka 2015 na 2016 na kwamba hadi sasa kilichobaki ni kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Akiongea na na East Africa Radio katika maojiano maalum mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema ajira za waalimu ni sawa na ajira za sekta nyingine, hivyo amewaomba waalimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi pale serikali itakapo tangaza utaratibu wa kutoa ajira mpya.
“Rais ametangaza utaratibu utakaotumika kutoa ajira mpya, hivyo amewaomba walimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi serikali itakapo tangaza kuanza kwa utaratibu huo” amesema.




