Jumapili , 14th Mei , 2017

Mwanasiasa maarufu Tanzania Edward Lowassa ameitaka serikali kutumia ubinadamu kufuatia sakata la kuwafukuza kazi wafanyakazi 9632 wenye vyeti feti, ambapo wamenyimwa mishahara pamoja na mafao yao.

Mhe. Edward Lowassa.

Lowassa alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam huku akiitaka serikali kuwa na moyo wa huruma katika kuwaadhibu wafanyakazi waliobainika kutumia vyeti feki.

Aidha Mhe. Lowassa alisisitiza kwamba hawatetei wenye vyeti feki, bali anatetea ubinadamu wao hivyo anaiomba Serikali kuwafikiria hao vijana na wazee waliotoa utumishi katika nchii kwa uaminifu.

"Kuwafukuza wafanyakazi  9632 kwa wakati mmoja, am not saying they are right, wala siwatetei, nauliza ubinadamu, watu hawa zaidi ya elfu tisa, wananyimwa mshahara na mafao yao waliyofanyia kazi miaka 20, 30 au 40 wataenda wapi? nakubali kuwa wamekosa sana ndio maana wananyimwa haki yao, lakini hata kama wamefanya kosa ilihitaji moyo wa huruma" -Mhe. Lowassa

Hata hivyo Lowassa ameipongeza Serikali kwa jitihada zake nzuri kwa kusema "Naipongeza Serikali kwa jitihada zao nzuri lakini katika hili nawaomba wawafikirie hawa vijana na wazee waliotoa utumishi katika nchii hii kwa uaminifu" - Mhe.Lowassa