
Prof. Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bahi Omary Badueli CCM aliyetaka serikali kutoa maelezo ya kuweza kuwalipa watu ambao udongo wao na changarawe hutumika kutengenezea barabara wawe wanalipwa fidia.
Aijibu swali hilo Prof. Mbarawa amesema kwamba serikali haina uwezo huo wa kulipa gharama za udongo na changarawe bali italipa kwa wanaovunjiwa nyumba na wenye ardhi zinazipitiwa na ujenzi lakini siyo kulipia fidia ya udongo unaotumika.
''Hatuwezi kuanza kununua udongo na changarawe, tutashindwa kujenga barabara, kilomita moja tu ya barabara huchukua shilingi bilioni moja hivyo tukianza kiulipia na fidia ya udongo wa kutumia tutakwama'' Amesema Prof. Mbarawa