Ijumaa , 1st Feb , 2019

Spika wa Bunge, Job Ndugai amepewa siku 14 kuwasilisha utetezi juu ya madai yaliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe juu ya mamlaka ya kikatiba ya kumuita Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) Profesa Mussa Assad.

Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) Profesa Mussa Assad, Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama kuu ya Tanzania, wakati ikisikiliza kwa mara ya kwanza kesi hiyo ya Kikatiba iliyofunguliwa na Zitto Kabwe ambapo mahakama imepanga kuisikiliza rasmi Februari 15.

Katika kesi hiyo, Zitto Kabwe kupitia wakili wake Fatma Karume atatoa hoja zake na wadaiwa ambao ni Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), watatoa utetezi wao kwa kujibu hoja hizo.

Shauri hilo linasilikizwa na Majaji watu Firmin Matogolo, Benhajj Masoud na Elinaza Luvanda ilitajwa ambapo hapo jana kupitia Wakili wa Serikali, Alesia Mbuya aliomba kuongezewa muda wa kuwasilisha maombi hayo.