
Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Gondwe ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakato alipokuwa akizungumza na EATV mara baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Saccos hizo na kusema kuwa wamebaini kuna saccos nyingi ambazo hazipeleki wakaguzi wa mahesabu yao na hivyo kuzua mtafaruku kwa wanachama.
Mkuu huyo wa wilaya ameziagiza saccos hizo kupeleka mahesabu ya taasisi zao kwa kila mwezi katika idara za ushirika na kuongeza kuwa endapo hawatawasilisha kwa muda wa miezi mitatu basi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zinazounda saccos hizo.
“Naagiza saccos zilizopo Temeke pia kuhakikisha zinakuwa na mkaguzi wa hesabu wa ndani ili kila baada ya miezi mitatu anafanya ukaguzi wa fedha hizo” amesema Gondwe.