Jumapili , 13th Aug , 2023

Rais wa Kenya William Ruto, amesema yuko tayari kufanya lolote ili kuhakikisha anatimiza lake la kutengeneza mazingira mazuri ya vijana nchini humo kupata ajira.

Rais wa Kenya William Ruto

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 13, 2023, kwenye ibada ya Jumapili jijini Nairobi na kusisitiza kwamba serikali yake tayari imeanza kufanya jitihada za makusudi kutoa fursa hizo kwa vijana  mpango ulioanzia kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu nchini humo.

"Watu wengi wamekuwa wakishangaa kwanini nasisitiza sana kuhusu hii ajenda ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu?, sisi nyumba tunazo nani kakuambia tunao uhitaji wa hizi nyumba?, lakini mimi lengo langu mimi si nyumba tu bali ni kuzalisha ajira kwa vijana wa Kenya," amesema Rais Ruto.