Rais wa Haiti auawa kwa shambulio

Jumatano , 7th Jul , 2021

Rais wa Haiti, Jovenel Moïse ameuawa katika shambulio ambalo limefanywa kwenye makazi yake Port-au-Prince.

Aliyekuwa Rais wa Haiti Jovenel Moïse.

Waziri Mkuu wa mpito wa taifa hilo Claude Joseph ambaye ndio anaongoza taifa kwa sasa amesema watu waliofanya shambulio hawajatambulika haswa ni kina nani ila ni wanajeshi wanaume.

Aidha ameeleza kuwa katika shambulio hilo mke wa Rais Jovenel Moïse pia amejeruhiwa na anaendelea kupatiwa matibabu.