Jumanne , 13th Jun , 2023

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka wakulima nchini kutokuuza mazao yao nje ya nchi kwani serikali inatarajia kununua tani laki tano kwa mwaka unaoanza kama hatua ya kudhibiti upungufu wa chakula nchini na mfumko wa bei unaoendelea duniani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 13, 2023, mkoani Mwanza wakati wa ufunguzi wa tamasha la Bulabo linalofanyika baada ya mavuno ambapo amesema kufuatia mfumko wa bei unaoendelea duniani wamechukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata unafuu.

"Kuendana na mfumuko huo wa bei sisi Tanzania tulipopata mfumuko wa bei kwenye mafuta tuliweka ruzuku yakawa na bei ya kawaida, kwenye mbolea tuliweka ruzuku na mambo yakawa sawa, na hadi sasa nchi yetu tumeenndelea sana kuzuia mfumuko wa bei kwenye chakula," amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia amezitaja sababu zilizopelekea dunia kuwa na tatizo la upungufu wa chakula ikiwemo tatizo ya Uviko19, vita vya Ukraine na mabadiliko ya tabianchi.