Ijumaa , 2nd Aug , 2024

Rais Samia amesema kwamba ufunguzi wa daraja la Berege lililopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, utasaidia kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Morogoro pamoja na Tanga, huku akiwashukuru wananchi kwa bango waliloliweka likisomeka kwamba hawana kitu wanachomdai.

Rais Samia

Hayoameyabainisha leo Agosti 2, 2024 mkoani humo wakati akiendelea na ziara yake ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Lakini kilichonifurahisha ni lile bango moja nililoliona linasema hatukudai uliyotuahidi umeyatekeleza," amesema Rais Samia

Kwa upande wao wananchi wa Berege wamesema kuwa daraja hilo limeleta matumaini mapya kwani litawanufaisha kiuchumi, kielimu, afya pamoja na kilimo