Jumamosi , 25th Jun , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza Mikopo kwa vikundi maalumu ibaki asilimia 10 tofauti na mapedekezo ya Bajeti kuu yaliyotaka iwe asilimia tano

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa fedha za mikopo kwa wanawake ,Vijana na Walemavu kutoka kwenye mapato ya Halmashauri zibaki kuwa asilimia 10 tofauti na mapendekezo yaliyotaka zibaki asilimia 5.

Dk.Mwigulu ameyabainisha hayo jana Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amesema Rais amesisitiza wananchi wasikilizwe kwanza kwakua ndio wamewaagiza wabunge wawaseme Bungeni hapo, huku Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza serikali kupitia fomu za maelekezo ya michango mashuleni kupunguzwa ili kuounguza mzigo kwa wazazi na wanafunzi.

Katika muendelezo wakujibu hoja za Wabunge leo ili kupitisha Bajeti hiyo ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Jenister Mhagama ameagiza kutumika kwa database ya Utumishi ili watanzania wengi waweza kupatiwa ajira na kuhifadhi kumbukumbu sahihi ambazo zitaboresha utumishi ,huku Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe akisisitiza bei za mbolea hazitawaumiza wakulima kama ilivyokua ikisemwa nakuwatoa hofu wakulima.