Jumamosi , 15th Jan , 2022

Jeshi la Polisi nchini, limetoa angalizo juu ya uwepo wa watu wanaotumia mitandao Kutapeli kwa kutengeneza vikundi na kuandaa maonyesho feki ama kuuza magari kwa mwamvuli wa serikali au picha ya kiongozi na kisha huomba mhusika kutuma ada ya ushiriki ama malipo na atakayetuma hutapeliwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi hilo, SACP David Misime, na kusema hadi sasa baadhi ya wahalifu wanaofanya vitendo hivyo wameshakamatwa na wengine bado wanaendelea kutafutwa.

"Huwatumia wanaowalenga kuwatapeli picha za mabanda ya maonesho, bidhaa au magari ili kuwaaminisha kuwa kuna maandalizi ya maonyesho yanaandaliwa na baada ya kufanya hivyo huwataka walipie ada ya ushiriki au walipe bidhaa hizo," amesema SACP Misime.