Jumatano , 28th Jun , 2023

Ernest Ryoba mwenye umri 61 mkazi wa Bula Kijiji cha Namanyere, Kata ya Majimoto wiaya ya Mlele mkoani Katavi amenusurika kifo baada ya kumwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali maeneo ya usoni na kifuani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani,

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani, amesema kwamba Ryoba alimwagiwa tindikali hiyo majira ya usiku wakati akitoka kwenye shughuli zake na waliomfanyia unyama huo kutokomea kusikojulikana.

Aidha jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wawili Vicent Yoshi miaka 23 na Hassan Masoud 32 kwa kosa la kukutwa na Televisheni mbili radio na baiskeli wakiwa wamevihifadhi kwenye nyumba wanazoishi.