Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Jumanne Muliro, na kusema kwamba watakaokiuka watachukuliwa hatua, na kwamba limebaini uwepo wa watu wanaouza tiketi bandia licha ya tiketi zote za tamasha hilo kuuzwa (Sold out).
"Jeshi la Polisi linazo taarifa kuwa kuna makundi ya watu wanazo tiketi za bandia na sasa wanaanza kuziuza kwa baadhi ya watu, Jeshi la polisi linawatahadharisha watu kuwa makini na kuuza ama kununua tiketi hizo, kwani linafuatilia sana kwa makini kundi la matapeli hao, hata hivyo ulinzi umeimarishwa siku moja kabla," amesema Kamanda Muliro