
Kamanda Lazaro Mambosasa
Kamanda Mambosasa amesema, mtuhumiwa huyo alikamtwa baada ya kukataa wito wa polisi ambapo awali aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano, lakini alikaidi kutii wito huo na kusema kwamba, jeshi la polisi linapomuita mtu kwa hiari na akaacha kutii wito huo, hutumia mbinu ya kumlazimisha atii.
''Baada ya kukamatwa mwandishi huyo, tulisikia taarifa mbalimbali kutoka kwa kada mbalimbali kwenye jamii wakiendelea kusema mwandishi huyo alitekwa niseme kuwa, mwandishi huyo hakutekwa aliitwa, lakini kwa jeuri alikaidi kutii wito huo, sababu pia ya kuitwa ni kuhusiana na utata wa uraia wake, Jeshi linaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na maafisa wa uhamiaji'', amesema SACP Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa, baada ya upelelezi kukamilika jeshi hilo litahakikisha kosa analotuhumiwa nalo mwandishi huyo, linawekwa mezani ili na yeye aweze kuhakikishia kama ni mtanzania kwa kutoa vielelezo vinavyothibisha uraia wake.