
Marehemu Emmanuel Polycupy Mlelwa.
Akiwa kwenye mkutano wake na waandishi leo Septemba 27, Polepole amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimefuatilia jambo hilo kwa uchungu mkubwa.
“Tunafahamu, sitaki kusema ili nisiingilie upelelezi wa polisi wamefanya mawasiliano na huyu kijana, wameomba kukutana naye, wakamteka, wamepotea naye tumekuja kukuta mwili wa kijana huyu eneo la Kibwena bwawani, amepigwa ameumizwa, amepoteza maisha yake" alisema Polepole
Aidha Polepole ametoa rai kwa jeshi la polisi kufanya upelelezi huku akisema kuwa hawako tayari kufanya siasa kwenye nchi hii inayomwaga damu.
“Sisi CCM tumefuatilia natunatoa rai kwa jeshi la polisi tafadhali wakati mwingine upelelezi unachukua muda bila sababu ya msingi, kipindi hiki ukweli unajulikana hatuko tayari kufanya siasa katika nchi hii tunamwaga damu nakupoteza maisha ya watanzania akiwemo kijana huyu mdogo” alisema Polepole