
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Kunisaga amesema kwamba wilaya hiyo ilikuwa na uhitaji wa madawati 8,048 ambapo hadi sasa wameweza kutengeneza madawati 3,432 ambayo yamepelekwa kwatika shule mbalimbali.
Kunisaga ameongeza kuwa madawati mengine 3,570 yanaendelea na matengenezo katika chuo cha ufundi Buhongwa na uhakika wa kukamilika upo.
Upungufu ambao upo ni wa madawati 1,016 ambayo hayajaanza kutengenezwa kabisa kutokana na ukata, hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ameomba msaada wa wadau wote wa elimu ili kuweza kukamilisha kazi hiyo ili kumaliza kabisa tatizo la madawati.