Tume hiyo imelitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wote wanaohusika na kutoa taarifa za uongo zinazosababisha taharuki katika jamii.
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma juu ya matokeo ya uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyo, mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini Jaji Mstaafu, Mathew Mwaimu, amesema uchunguzi ulihusisha maeneo yote yaliyotajwa katika Mikoa ya Dodoma, Singida na Kilimanjaro na kubaini ukweli juu ya kifo cha mwanafunzi huyo
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa inaeleza kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea Mei 1, 2023 katika hospitali ya Faraja iliyopo Himo, mkoani Kilimanjaro