
Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo (kulia) akiwa na wakili wake.
Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa 'WhatsApp' kuwa yupo hatarini, kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
Baada ya mahakama kutoa umamuzi huo leo Agosti 27, 2018 mshtakiwa Nondo atawatumia mashahidi watano kujitetea na kesi hiyo itasikilizwa tarehe 18 na 19 mwezi ujao.
Awali Mahakama ilishindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wawili kati ya watano wa kesi hiyo baada mshitakiwa kuiandikia barua Mahakama akimtaka Hakimu John Mpitanjia anayesikiliza kesi yake ajitoe kwa sababu ya kupoteza imani naye.