Jumatano , 20th Jul , 2022

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Nigeria (NCDC) kimesema kuwa kipo kwenye tahadhari kufuatia visa vya ugonjwa wa Marburg nchini  Ghana,  baada ya kuripotiwa visa viwili vya  nchini humo

Ugonjwa huo umetokea kwa watu wa familia moja nchini Ghana na inaelezwa ni ugonjwa ambao ni hatari kwani virusi vyake ndivyo vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola.  

NCDC imesema kuwa Nigeria imejidhatiti na kwamba inayo mifumo thabiti ya kudhibiti ugonjwa huo.  
Vikosi vya afya nchini humo vimewekwa tayari kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo muda wowote  
Mpaka sasa hakuna taarifa iliyoripotiwa kuhusu ugonjwa huo ndani ya Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika .  

Ghana imethibitisha uwepo wa ugonjwa huo hatari mapema wiki hii, huku wagonjwa wote wakipoteza maisha na wale waliokua karibu nao wakiwekwa karantini huku baadhi yao wakiruhusiwa kurejea majumbani mwao.