Alhamisi , 1st Dec , 2022

Serikali ya Nigeria imetangaza sera inayolenga kukuza ufundishaji wa wanafunzi wa shule za msingi kwa lugha za kizawa badala ya Kiingereza. 

 

Waziri wa Elimu wa Nigeria Adamu Adamu amesema kwamba  mfumo huo mpya unaojulikana kama Sera ya Lugha ya Taifa umeidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji.

Inaeleza kuwa mafundisho kwa miaka sita ya kwanza katika shule za msingi yatakuwa katika lugha mama. Kiingereza ni lugha rasmi ya Nigeria na taasisi zote za kujifunzia huitumia kama lugha ya kawaida ya kufundishia na kujifunzia.

Lakini lugha za wenyeji sasa zitachukua hatamu kwa sasa kuanzia ngazi ya shule za chekecheka, huku waziri wa elimu akisema  wanafunzi hujifunza vizuri zaidi wanapofundishwa kwa lugha yao ya mama.

Alikiri kuwa utekelezaji wa sera hiyo mpya utakuwa na changamoto kwa sababu "itahitaji kazi kubwa ya kutengeneza vifaa vya kufundishia na kupata walimu"..