Baraza limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.
Aidha Baraza hilo limesema litatangaza matokeo hayo baada ya taratibu za Wizara kukamilika hivyo wananchi wawe na utulivu.





