Ramadhani Kailima - Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC
Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo hiyo Ramadhani Kailima ametoa wito huo leo wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi pamoja na wasimamizi wasaidizi watakaoshiriki kusimamia uchaguzi mdogo utakaofanyika katika jimbo moja na kata mbalimbali nchini ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na waliokuwa madiwani na mbunge.
Alisema katika moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikileta shida wakati wa uchaguzi ni zoezi la kuhesabu kura pamoja na kutangaza matokeo hali inayosababisha kuzuka kwa vurugu maeneo mengi.
Aidha, aliwataka wasimamizi watakaoshiriki katika uchaguzi huo, kuhakikisha matokeo yanatakangazwa mapema ili kuondokana na vurugu ambazo zinaweza kutokea.
Kailima akizungumza na wasimamizi wa uchaguzi
“Katika hili, kumekuwa na changamoto kubwa sana kwani watu wanahitaji kupata matokeo lakini wasimamizi wanachelewesha kuyatangaza kiasi ambacho vurugu zinazuka vituoni kwa kutokuwa na imani nanyi, nawaombeni kuhakikisha hata kama matokeo hamjayatangaza kwa wananchi, lakini muwaeleze ili kipi kinasababisha kuchelewesha wala siyo kukaa kimya kiasi cha kuwatia mashaka wananchi,” alisema Kailima.
“Siku hiyo pia niwaombe kuhakikisha mawakala wa vyama vyote shiriki, wanakula kiapo cha kutunza siri na kama mtu atakataa, basi asipewe nafasi ya uwakala katika kituo cha uchaguzi kwani hayo ni matakwa ya kanuni na lazima ajaze fomu ya kutunza siri,” alisema.
Jumla ya kata 22 zinatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo nchini Januari 22, mwaka huu, katika nafasi za udiwani pamoja nafasi ya ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar.





