Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai
Akizungumza mara baada ya kiapo cha Prof. Manya jijini Dodoma leo, Ndugai amempongeza mbunge huyo kwa kuteuliwa kuwa mbunge huku akisema bunge hilo haitaki kurudisha nyuma kasi ya serikali.
“Nitoe wito kwa wabunge wengine wowote wale, kumbukumbu zangu zinaonesha kuna wabunge wanne wa ACT Wazalendo ambao bado hawajaapa ningetoa wito kama wenyewe wakiwa tayari kutumikia nchi yao kama kweli waliomba ubunge kutumikia wananchi hawana sababu ya kuzurura huko walipo watoe taarifa kwa spika haraka tuwapangie ili wapate kiapo waweze kufanya kazi ya mbunge” amesema Ndugai
Uapisho wa Prof. Shukrani Manya unakuja mara baada ya uteuzi wa Rais uliofanyika leo tarehe 11/12/2020 ambapo amemteua kuwa Naibu Waziri wa Madini na Mbunge mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

