Ijumaa , 7th Mei , 2021

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa licha ya aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia CHADEMA Tundu Lissu, kukaa Bungeni kwa muda wa miaka 10 lakini hakuwahi hata kutengeneza chanzo cha maji kijijini kwake Mahambe.

Kushoto ni Spika wa Bunge Job Ndugai, na kulia ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia CHADEMA

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 7, 2021, Bungeni Dodoma, mara baada ya mbunge wa jimbo hilo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu, kuomba kupelekewa maji wilayani Ikungi, kwani wananchi wake wanakunywa maji ya kwenye madimbwi pamoja na Ng'ombe.

"Katika mchango wa Mh. Mtaturu ametaja vijiji kadhaa ambavyo havina maji, katika vijiji hivyo amateja kijiji kimoja kinaitwa Mahambe hicho kijiji ndicho anachotoka Mh Lissu amekuwa mbunge miaka 10 kijiji chake mwenyewe hata chanzo cha maji hakuna", amesema Spika Ndugai.