Alhamisi , 8th Sep , 2016

Ndege kadhaa za mizigo zilizopaswa jana kwenda Mogadishu nchini Somalia zimekwama kuondoka Jijini Nairobi zikiwa na mirungi yenye thamani ya shilingi milioni 50 za Kenya, kufuatia serikali ya Somalia kuzuia mirungi kuingia nchini humo.

Zao za miraa la nchini Kenya ambalo lina soko sana nchini Mogadishu.

Hata hivyo vyanzo kutoka uwanja wa ndege vimesema baadhi ya ndege zenye shehena ya mirungi zimeenda katika miji ya Kismayu, Puntland na Galkayo nchini Somalia zikiwa na mirungi licha ya zuio hilo.

Wafanyakazi wa baadhi ya kampuni zinazosafirisha mirungi Jijini Nairobi wameelezwa kutoripoti kazini siku ya jumatatu kutokana na kampuni hizo kutokuwa na kazi za kusafirisha mirungi nchini Somalia.