Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.
Wakizungumza mbele ya Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu,alipotembelea katika kituo hicho, wamesema kituo hicho kinatoa huduma za upasuaji mkubwa na mdogo lakini madaktari wanakuwa katika wakati mgumu wa kufanya shughuli zao kutokana na ukosefu wa maji.
Aidha, waziri alimpa nafasi Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, atolee ufafanuzi kero hiyo ambapo amesema kuwa alishamwagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Zacharia Nachoa, kuhakikisha wanatumia mapato yao ya ndani kuweza kutatua changamoto ya ukosefu wa maji.
Katika kutekeleza agizo la Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi huyo amesema kuwa tatizo ambalo lilikwamisha kutatua kero hiyo kwa wakati ni kutokana na kukwama kwa pampu katika kisima, hivyo jitihada zinafanyika ili kuweza kuitoa na kuangalia kama haijaungua, huku akiahidi kuwa mpaka kufikia Aprili 15 kazi hiyo itakuwa imekemilika.