Alhamisi , 9th Nov , 2023

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani humo kumtia nguvuni, Andrea Ngomeni, mkazi wa Kijiji cha Kambikatoto Chunya kwa tuhuma za kuuza eneo la pori la akiba la hifadhi ya msitu wa asili Rungwa.

Sehemu ya pori iliyokutwa imefyekwa

Homera ametoa agizo hilo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya baada ya kufika katika hifadhi na pori la Rungwa Two na kukuta sehemu ya  hifadhi imefyekwa kwa ajili ya kilimo na mifugo na kujulishwa kuwa eneo hilo limeuzwa kwa wafugaji kutoka wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

"Nawaagiza polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kumsaka huyu bwana Andrea akamatwe ili hatua zichukuliwe, maana haiwezekani watu wanajifanyia wanavyotaka," amesema RC Homera

Kwa upande wake Mkuu wa wlaya ya Chunya, Mayeka Simon Mayeka, esema uharibifu wa maeneo umekuwa ukifanywa na wananchi kutoka nje ya moa wa Mbeya na mara nyingi wamekuwa wakikaribishwa na wenyeji wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji wasioowanifu.