Jescah Mneli ambaye amekumbwa na tukio la kikatili kutoka kwa vijana watatu ambao ni wafanyabiashara wenzake kwa kumbaka na kisha kumkata mkono.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Jumamosi ya Aprili 04, 2024 ambapo mwanamke huyo alipokutana na vijana ambao ni wafanyabiashara wenzake kisha kuelekea kwenye shamba la viazi ili kupanga bei na ndipo vijana hao wakamkamata kwa nguvu mama huyo kisha kumbaka na kumkata mkono.
Bi. Jescah anaiomba Serikali na wadau wengine kumsaidia kupata haki zake na kumudu gharama za matibabau wakati huu ambao anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Seriani
Daktari Robert Julius ambaye anaendelea kumpatia matibabu mama huyo amesema kwa sasa anaendelea vizuri licha ya kuwa bado ana maumivu.