Waliouwawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na Mkazi wa Kiwanja kata ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na mwingine ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.
Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 31,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.
Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje.
Akizungumza na EATV Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiwanja mahali alipo kuwa akiishi mwalimu huyo Gideon Peter Kinyamagiha amesema walifika nyumbani kwa marehemu na walipoingia ndani walikuta sururu ikiwa na damu na marehemu wawili na mtoto wa kiume wa mwalimu huyo akiwa amejuriwa uongozi ulitoa
Kinyamagoha anasema baadaye waliotoa taarifa Polisi ambao nao walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi ambapo majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga kuthibitisha chanzo cha tukio hilo la kinyama