Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa upepo huo ulikuwa wa hali isiyo ya kawaida, huku ukionekana ukitoa moshi na miali ya moto, jambo lililowashangaza na kuwatia hofu wakazi wa eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, amefika kijijini hapo kushuhudia athari za maafa hayo. Ambapo amewapa pole waathirika na kuwataka wananchi kuzingatia tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa hali ya hewa ili kuepuka madhara zaidi katika siku zijazo.
Licha ya uharibifu huo mkubwa kwa makazi, hakuna madhara wala vifo vilivyoripotiwa miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho.