Jumatano , 20th Jun , 2018

Mbunge wa Geita Joseph Musukuma (CCM), amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina kujitafakari na kung’atuka kufuatia maofisa wa wizara hiyo kuingia bungeni bila ridhaa katika mgahawa wa Bunge na kupima samaki wanaodaiwa kuvuliwa haramu.

Pichani kutoka kulia ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma na
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina

Musukuma ametoa kauli hiyo leo Juni 20, 2018 bungeni Jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19 ambapo amekiri kuwa gari lake liliwahi kukamatwa limebeba samaki wakaombwa rula.

“Hii Wizara imekuwa na Mawaziri watano madaktari lakini leo tumeleta mgambo sijui shule ya aina gani kila siku nashangaa? ni vizuri tukakaguliwa vyeti, mtu ana elimu ya kuunga uunga unamkabidhi Taifa tutakuja kufa kwa kutafuta kiki”, amesema Musukuma.

Akitoa taarifa ya Serikali bungeni leo kuhusu kilichotokea jana, Mpina amesema ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za wizara ikiwamo operesheni sangara ambayo jana ilitendeka bungeni, itaendelea lakini kwa bahati mbaya utekelezaji huo haukuzingatia tararibu za Bunge.