
Wakizungumza na #EATV wananchi waliokuwa eneo la tukio wamesema kuwa Aneth kabla ya kuzama kwenye mto alikuwa anatoka kwenye masomo ya kujiandaa kwa ajili ya kujiunga kidato cha kwanza shule ya Sekondari Kalema wakiwa njiani akiwa na rafiki yake ndipo walianza kutafuta Senene nyikani.
"Mtoto alitoka nyumbani asubuhi kwenda shuleni na sisi tukawa tumeenda kwenye majukumu mengine taarifa za kuzama kwenye maji tulizipata mida ya saa 10 tukaja hapa tukaanza kuangaika na wenzetu lakini hatukupata mwili wa mtoto huyo japo kuna mda tuliuona ukielea kwenye maji na kupotea", Amesema baba mzazi wa Aneth.
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera wamesema kuwa bado wanaendelea na juhudi za kuuopoa mwili wa Aneth.