
Mama Getrude Rwakatare wakati wa buhai wake, kulia ni mwanaye Muta Rwakatare
Hayo ameyabainisha leo Aprili 20, 2020, wakati wa mazungumzo maalum na EATV, ambapo amesema kuwa kwa sasa wanafamilia watakaa na kujua mazishi yatafanyika kwa namna gani, huku wakishirikiana kwa pamoja na Serikali.
"Amefariki leo na alikuwa yupo Hospitali, alikuwa na matatizo kidogo ya presha, kwahiyo mpaka sasa hivi tunasubiri majibu kutoka kwa wataalam tujue amepatwa na tatizo gani haswa" ameeleza Mtoto wa Marehemu Mama Rwakatare.
Mheshimiwa Askofu Mama Getrude Rwakatare, amefariki Dunia Alfajiri ya leo, katika Hosptali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.