Wakati takribani miaka 20 imepita tangu kuanza kukauka kwa mto Ruaha Mkuu, licha ya kuhamisha mifugo, mwaka 2005 katika Bonde la Usangu, ili kuongeza matumiani ya kunusuru mto huo, lakini jitihada hizo mpaka sasa hazijafanikisha kurejeza mto katika hali yake ya awali.
Kwa sasa kazi nyingine ya kuchimba mikondo ya asili ya mito imeanza kufanyika, lakini mratibu wa miradi ya shirika la uhifadhi wa mazingira na wanyama WWF nchini Tanzania bwana Keven Robert akizungumza wilayani Mbarali mkoani Mbeya amesema ikolojia ya mito inayoingia katika mto Ruaha mkuu imeharibiwa sana na haiwezi kufikisha maji kwa kiwango kinachotakiwa
Zaidi ya hekta 40,000 za wakulima wadogo na wawekezaji wakubwa wa mashamba ya mpunga zinategemea kilimo cha umwagiaji katika Bonde la Usangu wilayani Mbarali katika mkoa wa Mbeya, afisa maji wa bonde la Rufiji bwana Idrisa Msuya anasema matumizi mabaya ya ardhi katika kilimo yameongeza mmonyoko wa ardhi na kuharibu mikondo ya mito
Mto Ruaha mkuu umekuwa tegemeo kwa kilimo cha mpunga, hifadhi ya taifa ya Ruaha na katika uzalishaji wa umeme bwawa la Mtera na Kidato, ingawa sawa juhudi za kuokoa mto huo zinategemea sana uwajibikaji, mazungumzo na maamuzi ya pamoja ya serikali katika wizara husika.