![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2017/09/05/std 7.jpg?itok=UjIr6N_o×tamp=1504602496)
Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani Dr Charles Msonde amesema maandalizi kwaajili ya mitihani huo umekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza karatasi za mitihani, fomu maalumu za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu kwaajili ya mtihani huo.
Aidha Msonde ametoa onyokali kwa wasimamizi wa mitihani, waalimu, wananchi na wamiliki wa shule watakao jaribu kufanya udanganyifu kuwa watachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kufungia shule zote zitakazofanya udanganyifu.
Masomo yatakayo tahiniwa ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa.