Jumatano , 8th Jun , 2016

Jeshi la Polisi Kikosi Maalum cha Usalama Barabarani limesema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la makosa ya barabarani kwa kipindi cha miezi mitano ya mwaka 2016.

Jeshi la Polisi Kikosi Maalum cha Usalama Barabarani limesema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la makosa ya barabarani kwa kipindi cha miezi mitano ya mwaka 2016 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2015.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, amesema kuwa wamebaini ongezeko la makosa zaidi ya laki mbili kwa mawaka huu katika kipindi hicho wakati mwaka 2015 kuliripotiwa makosa zaidi ya laki nne na hivyo kwa sasa kuwepo kwa ongezekoa la zaidi ya makosa laki saba.

Aidha, Kamanda Mpinga amesema kuwa jumla ya ajali za barabarani 14 zimeripotiwa kutokea tangu kuanza kwa huduma ya mabasi ya mwendo kasi ambapo zimesababisha vifo 9 na majeruhi 5 huku watuhumiwa 54 wakiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa ya kutumia barabara za mwendo kasi kinyume na sheria.

Jeshi la polisi linawataka wananchi wote kuwa makini wanapokuwa barabarani na wanavyotumia vyombo vya moto ili kuweza kupunguza ajali zinazoonekana kugharimu maisha ya watu wengi nchini huku likiwatajka wananchi kuacha mara moja kutumia barabara za mwendo kasi kwani barabara hizo ni maalum kwaajili ya matumizi ya mabasi hayo pekee.