Jumanne , 28th Oct , 2014

Wafanyakazi wa Halmashauri wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo ya kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupunguza hewa ya ukaa katika kujiandaa na mashindano ya usafi wa mazingira Duniani.

Moja ya Maeneo ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya siku mbili mratibu wa mafunzo hayo Bi. Teresia Olemako amesema katika Programu hiyo waliyoipa jina la Wasaa wa mazingira pia itawawezesha kutengeneza nishati mbadala ya umeme kwa kutumia Taka mbovu ili kukabiliana na hewa ya ukaa na mabadiliko ya Tabia nchini.

Kwa upande wake Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuweza kufanya vizuri katika mashindano hayo ya mazingira ambayo yatashirikisha nchini 18 Duniani.

Ndesamburo ameongeza kuwa kushiriki katika mashindano hayo licha ya kuitangaza nchi lakini pia kutatoa elimu tosha ya mikoa mingine kuweza kuiga mfano wa Moshi katika utunzaji wa mazingira.