Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mlinzi wa chuo cha Ruaha aiba gari chuoni hapo

Jumatano , 7th Dec , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, linamshikilia David Richard, ambaye ni mlinzi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha (RUCU), kwa tuhuma za kuiba gari aina ya Toyota Raum yenye mali ya mfanyabiashara Abraham Gasper mkazi wa Mkwawa mjini Iringa ambayo ilikuwa kwenye maegesho chuoni hapo.

Gari aina ya Toyota Raum lililokuwa limeibiwa na mlinzi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi, amesema mtuhumiwa huyo aliiba gari ikiwa kwenye maegesho chuoni hapo na ndipo mmiliki wa gari hiyo alipogundua wizi huo alitoa taarifa kituo kikuu cha polisi na msako kuanza na hatimaye mtuhumiwa alipatikana wilayani Kilolo akiwa na gari hiyo .

Katika hatua nyingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wanaojihusisha na matukio yakihalifu ikiwemo wizi wa pikipiki ambapo katika nyakati tofauti walikamatwa wakiwa na jumla ya pikipiki tisa.

HABARI ZAIDI