Jumatano , 23rd Apr , 2014

Mweyekiti wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki amewaagiza watendaji na viongozi mbali mbali wa jiji kuchukua hatua za kinga kabla ya athari mbalimbali kujitokeza.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecky Sadiki

Sadiki ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam ametoa kauli hiyo leo jijini Dar-es-salaam wakati akifungua kikao maalum cha kamati ya Ushauri ya Mkoa RCC.

Kamati hiyo imekutana leo jijini Dar es salaam ikiwajumuisha Mameya, Wabunge , Wakurugenzi mbalimbali wa jiji na viongozi wengine ili kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza jijini Dar es salaam na namna sahihi ya kupatiwa ufumbuzi na kisha Mh. Meck Sadiki kutoa matokeo ya kikao hicho kesho kutwa.