Waziri wa fedha na Mipango Mh. Dkt. Philip Mpango.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa fedha na mipango Mh. Dkt. Philip Mpango wakati akisoma mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016,2017.
Aidha serikali imesema kuwa misaada pia inaweza kuchochea rushwa na kuzorotesha jitihada za ukusanyaji mapato na pia misaada kuondolea nchi kujiamini katika kujiamulia mambo yake yenyewe.
Sambamba na hilo Waziri wa Fedha na Mipango amesema kuwa suala lingine linalorudisha nyuma maendeleo ni wananchi wengi kutumia vibaya matumizi ya muda ambapo wengi wao wanatumia muda wa kazi kwa mambo yasiyo na tija.
Akiongela kuhusu Namna serikali inafikiria misaada ya ya wahisani Waziri wa Mambo ya nje na Afrika Mashariki Balozi Augustin Mahiga, amesema kuwa uamuzi huo ni mzuri kwani Masharti yamekuwa mengi katika nchi na serikali itakua tayari kwa misaada isiyokuwa na masharti ya kuikandamiza nchi.