
Watoto hao walibainika wamekufa maji majira ya saa nne usiku jana Septemba 13/2023 baada ya wazazi wao kurudi kutoka msibani usiku na kuanza kuwatafuta watoto wao,ambapo walikuta mwili wa mtoto mmoja unaelea juu ya maji kwenye bwawa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo watoto hao waliachwa nyumbani na wazazi wao na kwamba wakati wa zoezi la kuwatafuta alianza kupatikana mtoto mmoja na mwingine wakaendelea kumtafuta.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu ambaye ni Diwani wa Kata ya Mondo lilipotokea tukio hilo William Jijimya amesema, watoto hao waliachwa na wazazi wao nyumbani baada ya kwenda msibani kwenye kijiji cha Kabila.
Amewataja watoto waliofariki kuwa ni Meckline Dioniz (6) na Mbalu Dioniz (3) wa familia ambao wamefariki dunia baada ya kuzama katika bwawa la maji wakati wazazi wakiwa msibani.
Paschazia Emmanuel mkazi wa Kata ya Mondo amesema tukio hilo limewasikitisha kutokana na watoto hao kuondoka wakiwa bado wadogo ambao wangeweza kuja kusaidia wazazi baadaye.