Jumanne , 29th Mar , 2016

Imebainishwa kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kuwa ni chanzo kinachotoshia uzalishaji wa mazao na usalama wa chakula na kusababisha baa la Njaa.

waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba akimnyanyua mmoja wa waathirika wa mgogoro kati ya wafugaji na Wakulima

Mtafiti wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), Claude Maeda amesema migogoro hiyo imekua kikwazo kutokana na wakulima kushindwa kufanya shughuli za kilimo ili kuongeza uzalishaji.

Maeda amesema kuwa wakulima wengi licha ya kuwa na mshamba ya kilimo baadhi yao waekuwa wakishdnwa kufanya shughuli hizo kutokana na mazao kuharibiwa na mifugo na wanapoiondoa hushambuliwa na wafugaji hao.

Mchumi huyo ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo kuna haja serikali ya serikali kumaliza tatizo la migogoro hiyo ili wakulima waongeze uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Utafiti huo umefanywa na mradi wa Usalama wa Chakula(Trans Sec), kwa kushirikiana na mtandao wa vikundi vya wakulima(MVIWATA), walioufanya katika vijiji viwili vya wilayani Kilosa.